Luke 22:3-6

3 a bShetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale Kumi na Wawili. 4 cYuda akaenda kwa viongozi wa makuhani na kwa maafisa wa walinzi wa Hekalu, akazungumza nao jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Isa. 5 dWakafurahi na wakakubaliana kumpa fedha. 6Naye akakubali, akaanza kutafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Isa kwao, wakati ambapo hakuna umati wa watu.

Maandalizi Ya Pasaka

(Mathayo 26:17-25; Marko 14:12-21; Yohana 13:21-30)

Copyright information for SwhKC